Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Michezo


 
TIMU za Mali na Ivory Coast nazo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa Afrika 2015 kutoka Kundi D huku Guinea na Cameroon wakiyaaga mashindano hayo. Ivory Coast wakipongezana kwa ushindi dhidi ya Cameroon usiku huu. Mali wamesonga mbele baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Guinea huku Ivory Coast wakiwachapa Cameroon bao 1-0. Kwa matokeo hayo Mali na Ivory Coast… 



SIMBA YALALA KWA MBEYA CITY
SIMBA SC imeendelea kupoteza michezo yake hasa ya nyumbani baada ya leo kukubali tena kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imepigwa muda mfupi uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba hivi karibuni ilipoteza mechi yake ya nyumbani baada ya kupigwa na Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Azam FC majuzi.



ASAMOH AIKOA GHANA
 Ghana walifungua wazi Kundi C fainali za Kombe la Taifa Bingwa Afrika walipojipatia ushindi wa 1-0 dakika za mwisho dhidi ya Algeria uwanja wa Estadio de Mongomo Ijumaa jioni.
Asamoah Gyan, aliyerejea baada ya kuugua Malaria, alifungia Black Stars dakika ya mwisho ya mechi. Matokeo hayo yalipelekea taifa hilo la Afrika Magharibi kujiunga na Senegal (waliokuwa wacheze na Afrika Kusini baadaye Ijumaa) na Algeria katika kuwa na alama tatu kileleni mwa kundi hilo.Black Stars walifanya mabadiliko mawili kwenye kikosi kilicholazwa 2-1 na Senegal, badiliko muhimu likiwa kureja kwa Asamoah Gyan safu ya mashambulizi, na wakarejelea mpangilio wa 4-4-2.Mbweha wa Fennec nao walifanya mabadiliko matatu kwenye kikosi kilicholaza Afrika Kusini 3-1, Madjid Bougherra akiingia nafasi ya Rafik Halliche ulinzi, na washambuliaji Saphir Taider na Ishak Belfodil wakiingia.Algeria walianza wakionekana wenye nguvu kushinda Ghana, huku pasi zao fupi na ujeuri wakisonga vikiacha Ghana wakihangaika kukaa na mpira muda mrefu.
Vijana hao wa Afrika Magharibi waliunda nafasi murua ya kuanza kufunga dakika ya 20, Saphir Taider akichomoka kulia na kumfaa Nabil Bentaleb, lakini mchezaji huyo wa Tottenham Hotspur akatuma kombora lake nje.Nafasi hiyo ilikuwa ndiyo kuu pekee dakika za kwanza 45. Kipindi cha kwanza mchezo ulikuwa wa utepetevu na kujilinda sana timu zote zikionekana kuogopa kushambulialicha ya kuwa na wachezaji nyota.Ghana walianza kipindi cha pili wakionekana kuwa na uhai zaidi safu yao ya mashambulizi. Dakika ya 52, mkabaji wa kulia Harrison Afful alitoa krosi safi iliyomfikia Gyan, lakini straika huyo hakuweza kutikisa wavu.Wanaafrika Magharibi hao waliendelea kujiongezea uwezekano wa kufunga kipindi cha pili kilivyosonga, huku Algeria nao wakionekana hatari kwenye kaunta. Walidhihirisha hili dakika ya 66 kupitia nafasi iliyomwangukia kiungo wa kati Bentaleb ingawa hakuweza kulenga goli, na kombora lake likaenda nje.Mechi hiyo ilionekana kana kwamba ingeisha sare, lakini dakika za ushei mpira kutoka safu ya ulinzi ya Ghana ulimfikia Gyan na kwa ujanja mkubwa na kasi akamlemea difenda Carl Medjani na kisha kumbwaga kipa Rais Mbolhi na kufunga bao safi la ushindi. 

Ghana XI: Brimah, Afful, Rahman, Amartey, Mensah, Acquah, A. Ayew, Badu, Atsu, Gyan, J. Ayew

Algeria XI: M'Bolhi, Mandi, Bougherra, Medjani, Ghoulam, Lacen, Taider, Bentaleb, Brahimi, Feghouli, Belfodil


ZAMBIA YALALA 2-1 KWA TUNISIA


Tunisia ilichukua fursa ya kushindwa kwa Zambia kufunga mabao ya wazi ilipotoka nyuma na kuishinda miamba hiyo ya Chipolopolo 2-1.Mchezaji Emmanuel Mayuka alifungua ukurasa wa mabao katika mchuano huo baada kufunga krosi iliopigwa na Rainford Kalaba.Lakini Mayuka alipata jeraha na hivyobasi kutolewa alipojaribu kufunga bao la pili alipokuwa amesalia na wavu.Lakini Ahmed Akaichi alisawazisha katika eneo la hatari.Tunisia iliimarisha mchezo wake baada ya bao hilo na ilipofikia dakika ya 88 Yasine Chikhaoui alifunga bao la pili kupitia kichwa.Tunisia sasa ina alama 4 baada ya mechi mbili huku Zambia ikiwa na alama moja huku kukiwa kumesalia na mechi moja katika kundi B la michuano ya mataifa ya Afrika.



SAMATA KUKIPIGA ULAYA


Mbwana Samatta, tayari  akifanya majaribio na timu ya CSKA Moscow  ya nchiniUrusi.Mbwana amekosa kucheza mechi ya kwanza ya majaribio na Klabu hiyo baada ya kuumua Enka wakati akiwa kwenye mazoezi na timu hiyo, ambapo hata hivyo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo wa kirafiki.Hata hivyo Samatta, anatarajia kutua uwanjani kesho endapo atakuwa fiti kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, kwa ajili ya mechi ya pili ya kirafiki dhiti ya timu yake na FSV Frankfurt..

ALGERIA YAIBURUZA SOUTH 3-1



Algeria imeanza kampeni zake kwa kuruka juu kwa kuiadhhibu South Africa jumla ya magoli 3-1

SENEGAL YAIADHIBU GHANA 2-1
Mshambuliaji wa Senegal Moussa Sow alifunga bao la mda wa lala salama na kuisaidia Senegal kupata ushindi dhidi ya Black stars ya Ghana. Mchezaji huyo aliyeingia dakika za mwisho za mechi hiyo alifunga bao lake kunako dakika ya 90 na kuipatia timu yake alama zote tatu. Mchezaji wa Ghana Andrew Ayew alifunga mkwaju wa Penalti baada ya kiungo wa kati wa Everton Christian Atsu kuangushwa katika eneo la hatari. Lakini Senegal ilijitahidi na kupiga chuma cha goli la Ghana kupitia mchezaji Kara Mbodj,kabla ya mshambuliaji wa Stoke Mame Biram Diouf kufunga bao la kusawazisha huku Mousa Sow akifunga bao la Ushindi.

ZAMBIA VS CONGO SARE
MASHINDANO ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, yameendelea Leo baada ya Jana kuchezwa Mechi mbili za ufunguzi za Kundi A na Leo Zambia kutoka Sare 1-1 na Congo DR katIka Mechi ya kwanza ya Kundi B iliyochezwa Nuevo Estadio de Ebebiyín Mjini Ebibiyin.Zambia walitangulia kufunga katika Dakika ya Pili tu wakati Given Singuluma kumzidi Kipa wa Congo DRC Kidiamba, ambae wote huchezea Klabu ya TP Mazembe huko Lumbumbashi.Lakini Congo DRC wakasawazisha kwa Bao la Dakika ya 66 Yannick Bolasie anaechezea Klabu ya Ligi Kuu England, Crystal Palace.Baadae Leo itachezwa Mechi ya Pili ya Kundi B kati ya Tunisia na Cape Verde.

TUNISIA VS CAPE VERDE SARE
Mechi ya pili iliyoanza majira ya saa 4:00 usiku, miamba ya soka kaskazini mwa Afrika, Tunia ilitoka sare ya 1-1 na Cape Verde. Tunisia walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 70′ kupitia kwa Mohamed Ali Moncer, lakini dakika ya 78′ Cape Verde walisawazisha kupitia kwa Heldon aliyefunga kwa mkwaju wa penalti. Cape Verde, nchi inayotajwa kupata maendeleo makubwa ya soka duniani katika kipindi cha miaka miwili au mitatu iliyopita wameonesha ukomavu mkubwa katika mechi hiyo Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za mbili za kundi C kama inavyoonekana kwenye ratiba chini hapo chini; 19:00 Ghana vs Senegal 22:00 Algeria vs South Africa

EQUATORIAL GUINEA NA CONGO ZATOKA SARE
E.GUINEA-VS-CONGO
Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika imeanza rasmi kwa michezo miwili ya kundi A iliyochezwa kwenye siku ya ufunguzi (Jumamosi) ikizihusisha timu mwenyeji Equatorial Guinea na Congo Brazzaville pamoja na mchezo mwingine kati ya Gabon na Burkina Faso.
Katika mchezo wa kwanza Wenyeji Equatorial Guinea na Congo Brazzavile walitoka sare ya kufungana 1-1 katika mchezo uliokuwa mkali na wa kusisimua ambapo timu hizi zilishambuliana kwa karibu dakika zote za mchezo.
Equatorial Guinea ndio walioanza kufunga kupitia kwa nahodha wao Emilio Nsue Lopez ambaye alifunga kwenye dakika ya 16 baada ya kupokea pasi toka kwa Ivan Zarandona.


GABON WAIRARUA BUKINA FASO
Aubameyang akishangilia baada ya kuiungia Gabon bao la kuongoza katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Burkina Faso.
Aubameyang akishangilia baada ya kuiungia Gabon bao la kuongoza katika ushindi
wa 2-0 dhidi ya Burkina Faso.
Gabon walianza kufunga kwenye dakika ya 19 mfungaji akiwa mshambuliaji na nahodha wa timu hiyo Pierre Emerrick Aubameyang ambaye alifunga kwa shuti la karibu baada ya kuwapita mabeki.
Katika kipindi cha pili Gabon walifunga bao la pili kwenye dakika ya 72 mfungaji akiwa Malick Evouna akimalizia kwa kichwa mpira wa krosi uliopigwa na Frederic Bulot.
Matokeo haya yanamaanisha kuwa Gabon wanaongoza kundi A baada ya michezo ya kwanza wakiwa na pointi tatu huku Equatorial Guinea na Congo Brazzavil wakifuatia wakiwa na pointi moja kwa kila timu na Burkina Faso wanashika mkia wakiwa hawana pointi yoyote.


FACAO MAMBO MAGUMU


Mkolombia , anapata  £265,000  kwa wiki, amefunga magoli matatu katika uwepo wake mara  13 tangu asaini kutoka  Monaco kwa mkopo wa thamani ya  £6m September.
na hatimae kumnunua kwa £40.
"Atacheza katika klabu maaraufu msimu ujao , pengine Manchester
 United au la ," alisema wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka  28 Jorge Mendes.
Kiwango cha Facao kimeshuka kutokana na maumivu

TAKWIMU ZA FALCAO


Goals: 3 Total shots: 17
Appearances: 13 Shot conversion rate: 17.7%
Minutes played: 604 Assists: 3
Minutes per goal: 201.3 Chances created: 10



                                                     SAMATA KUKIPIGA ULAYA
 
 Huenda utakuwa ni mwaka wa neema kwa mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe kwa kuwa timu nne za Ulaya zimeonyesha nia ya kumchukua, ambazo ni kutoka katika nchi za Ufaransa na Italia, zimeonyesha nia ya kufanya kazi na mshambuliaji huyo Mtanzania. “Kweli tunayajua majina ya timu nne, kumekuwa na mawasiliano kupitia meneja wake Tanzania pamoja na uongozi wa TP Mazembe,” kilieleza chanzo kutoka Ufaransa. “Tusingependa kuanza kueleza kila kilichopo kwa sasa, lakini tunaamini Samatta anaondoka Mazembe msimu huu.” Baada ya taarifa hizo, juhudi zilifanyika kumpata meneja wake, Jamal Kisongo ambaye alitoa ushirikiano. “Kweli kuna timu zinamhitaji, kama nilivyokueleza awali Mbwana si mtu wa kwenda kufanya majaribio, badala yake kujiunga na timu na kuanza kazi. “Sasa kinachofanyika ni taratibu na nimekuwa na mawasiliano na uongozi wa TP Mazembe, hivyo vuteni subira kidogo,” alisema Kisongo akionyesha kujiamini kuhusiana na mchezaji wake huyo. Samatta yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko na amekuwa mchezaji tegemeo wa kikosi cha Mazembe. Awali ilielezwa, mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi, alikuwa akifanya juhudi kuhakikisha Samatta anabaki Lubumbashi, DR Congo, lakini Kisongo amehakikisha anakwenda mbele zaidi ili kupata mafanikio zaidi


SIMBA BINGWA MAPINDUZI


Timu ya Simba imetwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2015 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90.
Shujaa wa Simba SC alikuwa ni kipa Ivo Mapunda aliyetokea benchi dakika ya 90 kwenda kuchukua nafasi ya Peter Manyika na kuokoa penalti ya mwisho ya Mtibwa iliyopigwa na Vincent Barnabas.
Awali, Ivo alishuhudia penalti ya Ibrahim Rajab ‘Jeba ikigonga mwamba wakati upande wa Simba SC, penalti ya Shaaban Kisiga ‘Malone’ ilipanguliwa na kipa wa Mtibwa Said Mohammed Kasarama.
Penalti za Simba SC zilifungwa na Awadh Juma, Hassan Kessy, Hassan Isihaka na Dan Sserunkuma, wakati za Mtibwa zilifungwa na Aly Lundenga, Shaaban Nditi na Ramadhani Kichuya.
Kipa huyo wa Mtibwa ndiye ametajwa kipa bora wa mashindano, mchezaji bora Salim Mbonde wa Mtibwa na mfungaji bora Simon Msuva wa Yanga SC.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Peter Manyika/Ivo Mapunda dk90, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Juuko Murushid, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi, Said Ndemla/Shaaban Kisiga ‘Malone’ dk89, Ibrahim Hajibu/Elias Maguri dk65, Dan Sserunkuma na Emmanuel Okwi/Awadh Juma dk75.
Mtibwa Sugar kilikuwa; Said Mohammed, Ally Lundenga, David Luhende, Salim Mbonde, Andrew Vincent, Shaaban Nditi, Mussa Nampaka/Ibrahim Rajab ‘Jeba’ dk66, Muzamil Yassin, Ame Ally/Abdallah Juma dk90, Ally Shomary/Ramadhani Kichuya dk87 na Mussa Hassan ‘Mgosi’/Vincent Barnabas dk78.


CHRISTIAN RONALDO AIKWAA TUZO TENA


Kwa mara ya pili mfululizo, mchezaji wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amechaguliwa kuwa Mwanasoka Bora wa Dunia.
Ronaldo amewapiku washindani wenzake wawili kwenye Ballon d’Or, ambao ni Lionel Messi wa Barcelona na Argentina na kipa Manuel Neuer wa Bayern Munich na Ujerumani.
Ronaldo (29) amepata asilimia 37.66 ya kura zote na hii ni mara ya tatu anashinda tuzo hiyo. Messi aliyepata kuitwaa mara nne alipata 15.76%, akimzidi kidogo tu Neur aliyepewa 15.72%.
Ronaldo aliyefunga mabao 52 katika mechi 43 mwaka jana, alionekana mwenye hisia kali wakati wa kupokea tuzo yake kutoka kwa mchezaji wa zamani wa Arsenal, Barcelona na Ufaransa, Thierry Henry.
“Ningependa kuwashukuru wote walionipigia kura, rais wangu, kocha wangu na Real Madrid, umekuwa mwaka ambao hautasahaulika. Kutwaa tuzo hii hatimaye ni kitu cha pekee kabisa,” akasema Ronaldo.
Kiungo wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez ametuzwa kwa kufunga bao zuri zaidi kwa 2014 wakati Kocha wa Ujerumani, aliyetwaa Kombe la Dunia, Joachim Low ametangazwa kwua kocha bora wa dunia.
Washindani wale watatu wa Ballon d’Or wamejumuishwa kwenye Timu ya Dunia, pamoja na mabeki Philipp Lahm, David Luiz, Thiago Silva na Sergio Ramos.
Viungo wa kikosi cha dunia ni Andres Iniesta, Toni Kroos na Angel Di Maria wakati mshambuliaji mwingine ni Arjen Robben.


TOURE TENA AFRIKA

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City, Yaya Toure afanikiwa kutwaa tuzo ya mwanasoka bora wa bara la Afrika kwa mara ya nne mfululizo.
Tuzo hiyo inayotolewa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF), imeshuhudia Yaya Toure akiwapiku wachezaji wawili, Pierre Emerick Aubameyang (Gabon) na golikipa wa timu ya taifa ya Nigeria, Vicent Enyeama.
Yaya alipata kura 175 dhidi ya mshambuliaji wa klabu ya Borrusia Dortmund, Aubemayang aliyejinyakulia kura 12o huku Enyeama akiangukia nafasi ya tatu kwa kupata jumla ya kura 105.
Katika hatua nyengine tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kutoka katika ligi za ndani imekwenda kwaFirmin Mubele Ndombe wa AS Vita huku ile ya mchezaji bora wa kike akinyakuliwa na Asisat Oshoala anayekipiga katika klabu ya River Angels.

No comments:

Post a Comment