WEMA AFUNGUKA KUHUSU KUMDAI DIMOND
Ukubwa wa stori hii ambayo jana aliizungumzia Martin Kadinda kama Meneja
wa Wema Sepetu i Wema
amesema,Taarifa hii imenishtua sana maana asubuhi ya jana
nimekuta kwenye gazeti wameandika nikashangaa yaani hapa nimekaa kwa
sababu muda mwingi siendeshi mimi akaunti yangu ya twitter,anaiendesha
mtu wangu wa blog Bestizo maana nilikua nataka kutoa tamko’‘Nilishasema
ukurasa huu tulishaufunga na nilishasema haiwezi kujirudia
tena,nashangaa watu wanarudi na maneno yale yale maana nimekaa kimya kwa
kila kitu ili kuepuka haya maneno’‘Hakuna kitu ambacho namdai
Diamond,hakuna siku hata moja nimefikiria kwenda kumshtaki Diamond labda
kama kungekua kuna kitu chochote,yaani labda kungekua na ukweli wa kitu
chochote siwezi kupoteza muda wangu kwenda polisi,sijawahi kufanya kitu
cha namna hii hizi taarifa zimenishtua sana’‘Sijawahi kujiunga Vikoba
maana sivijui,nilikua nimekaa na mtu akanambia labda Wema hujui hawa
watu wa vikoba wanajaribu kujitangaza kwa njia hii na kutengeneza hii
kitu kwamba vikoba wanaweza kukopa hadi Milioni kumi kwanza mimi siwezi
kukopa Milioni 10′
WEMA HAMDAI DIMOND
Martin ameiambia Bongo5 kuwa Wema na Diamond hawadaiani chochote na kwamba habari hizo ni za uongo.
“Unajua tatizo ni kwamba hatujajua source ni nani,” amesema Martin. “Kwa sababu taarifa ikishaingia kwenye social network everybody posts, kwahiyo sisi tunamtafuta nani ameianzisha hiyo stori. “We don’t have any issue with Diamond. Diamond hana issue yoyote na Wema,” amesisitiza.
“Kwahiyo tunashangaa ni kama ambavyo wanazusha sijui kafumwa na nani ni uongo mtupu. Lakini nashangaa media ambazo zinaaminika zinaamua kuandika story bila kumpigia simu mhusika au meneja na kuuliza ukweli wa hiyo story.”
WEMA BOB JUNIOR MAPENZI MOTO
Kwa mujibu wa habari za chini ya pazia inasemekana kuwa Msanii Bob Junior anatoka na Wema Sepetu
CHAMELEONE AMPA KICHWA DIAMOND
Muimbaji wa Uganda, Jose Chameleone ameuzungumzia uhusiano kati ya Zari Ttale na Diamond Platnumz ambao kwa sasa umekuwa maarufu mno Afrika Mashariki.
Akizungumza na mtandao wa Kenya, Ghafla, Chameleone alisema haoni kama kuna tatizo kwa mastaa hao kuwa wapenzi. “Kama wanapenda, hakuna tatizo,” alisema muimbaji huyo wa Valu Valu.
“Diamond hajaoa na Zari pia hajaolewa. Kuwa na uhusiano wa zamani hakumzuii (Zari) kuwa na uhusiano mwingine.”
Kauli hiyo ya Diamond imekuja siku chache tu baada ya Diamond kutangaza kuwa yeye na Zari wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza.
Kwa upande mwingine alipoulizwa kuhusu Diamond kama msanii, Chameleone alisema: Ni msanii mzuri pia. Namba ya wasanii wazuri Afrika Mashariki inazidi kukua. Ndio maana muziki wetu umeanza kuchezwa Nigeria sababu nguvu ni kubwa kutoka Afrika Mashariki.”
No comments:
Post a Comment