Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Friday, 23 January 2015

DAR KUKOSA MAJI SIKU MBILI




Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48  kwa siku za Ijumaa na Jumamosi ya tarehe 23 na 24 January 2015, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (cross-connection) katika mtambo wa Ruvu Chini eneo la Chambezi, Bagamoyo. Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; 
Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe. 
Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.       
Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.

Au piga simu huduma kwa wateja namba 022- 2194800  / 0658-198889

Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

No comments:

Post a Comment