Polisi Tanzania linamshikilia
mwenyekiti wa chama cha siasa cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba na
wakiwemo wafuasi wake 32 pia kwa tuhuma za kufanya maandamano
yanayodaiwa kuwa si halali.
Inadaiwa kuwa polisi hao awali
walizuia maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika kama sehemu ya
maadhimisho ya kukumbuka ya miaka 14 tangu kufanyika kwa mauaji na
mateso kwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara.
Naibu
Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro ameiambia BBC kuwa
wanamshikilia mwenyekiti huyo wa Chama cha siasa cha CUF na kwamba kati
ya hao 32 wanaoshikiliwa wawili ni wanawake.
Polisi kwa mjibu wa
Siro wanasema walikwisha waandikia barua barua viongozi wa chama hicho
cha CUF kupinga kufanyika kwa maandamano hayo kwa sababu za kiusalama
Mwak 2001 chama cha CUF visiwani Zanzibar waliendesha maandamano yaliyosababisha baadhi ya Polisi na raia kadhaa kufa.
No comments:
Post a Comment