Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Monday, 19 January 2015

SENEGAL YAPIGA MARUFUKU JARIDA LA CHARLIE HEBDO

 

Senegal imepiga marufuku usambazaji wa jarida hilo kote nchini humo
Raia wengi wa Senegal ni waisilamu ambao bila shaka watafurahishwa na hatua hii ya serikali.
Nchi hio pia ina uhusiano wa karibu na Ufaransa ambayo ilikuwa mkoloni wake na majarida mengi ya kifaransa yanapatikana nchini humo.
Jarida hilo limesambazwa kote duniani likuwa na kibonzo kinachomkejeli mtume akionekana kulia huku akishika bango linalosema ''Mimi ni Charlie'' huku kichwa kinachofuata kikisoma, '' Yote yamesamehewa''.
ni hatia kwa yeyote kusambaza au kuchapisha kibonzo kilicho kwenye jarida la Charlie Hebdo kote nchini,''ilisema taarifa ya shirika la habari la APS likinukuu taarifa kutoka kwa wizara ya mambo ya ndani.
Mwandishi wa BBC nchini humo, Mamadou Moussa Ba anasema hakuna cha kushangaza kuhusiana na marufuku hio.
Raia wengi wa Senegal wamemkosoa rais Macky Sall kwa kuhudhuria maandamano nchini Ufaransa kuonyesha umoja kufuatia mauaji ya wachora vibonzo wa Charlie Hebdo na vijana waisimalu waliosema kwamba walikuwa wanalipiza kisasi kibonzo kilichochorwa awali na jarida hilo pia kumkejeli mtume.
Gazeti moja nchini Kenya, la The Star limeomba radhi kwa kuchapisha ukurasa wa kwanza wa jarida la Charlie Hebdo uliokuwa na kibonzo kinachomkejeli mtume Muhammad.Wahariri wa gazeti hilowamesema kuwa wanaomba radhi ikiwa walimkera mtu yeyote kwa kuchapisha ukurasa huo. Malalamiko kutoka kwa viongozi wa kiisilamu yalipelekea wahariri wa gazeti hilo kuomba radhi.


No comments:

Post a Comment