Akithibitisha taarifa hizo Spika wa Bunge Mh. Anna Makinda amesema kuwa
kwa mujibu wa maazimio ya Bunge, wenyeviti hao walipaswa kuwajibika mara
moja katika kamati zao, na kwamba sio jukumu lake kuwaondoa katika nafasi hizo kwa kuwa walichaguliwa katika kamati zao.
Amesema yeye anapokea taarifa kutoka ndani ya kamati kuhusu uwepo wa
mwenyekiti au la, ili atoe ruhusa ya kufanyika kwa uchaguzi wa
mwenyekiti mpya lakini anachojua ni kwamba hadi sasa wenyeviti hao
tayari wamejiuzulu nafasi hizo.
Wenyeviti hao ni Wiliam Ngeleja aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya
Sheria, Katiba na Utawala aliyetajwa kupokea pesa kutoka kwa James
Rugemalira, Andrew Chenge aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya Bajeti
ambaye pia anatajwa kupokea fedha kiasi cha shilingi Bilion 1.6 kutoka
kwa James Rugemalira.
Mwingine ni Victor Mwambalaswa aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya Nishati
na Madini ambaye pia alikuwa katika bodi ya TANESCO inayodaiwa kuhusika
kwa kiasi kikubwa katika sakata la fedha zilizokuwa katika akaunti ya
Tegeta Escrow.
kamati hiyo iko chini ya makamu mwenyekiti Bulugu Festus Limbu
kamati hiyo iko chini ya makamu mwenyekiti Bulugu Festus Limbu
No comments:
Post a Comment