Wezesha
kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com
Monday, 16 February 2015
BABA WA DULLY SYKES AAGA DUNIA
BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Dully Sykes, mzee Ebby Sykes amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Presha.
Ebby Sykes alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri na ndiye anayedaiwa kumfundisha mambo mengi ya muziki mwanae Dully Sykes.
Sykes alizaliwa February 24, 1952 ambapo tarehe hiyo mwaka huu alikuwa anatimiza miaka 63.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
-Amen
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment