Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa Kapteni John Komba amefariki dunia katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam.Mpaka kufa kwake Kapteni John Komba alikuwa Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi na Mjumbe wa Halmasauri Kuu ya CCM Taifa na Kiongozi wa bendi ya TOT.
Komba inadaiwa amefariki Baada ya kupandwa na sukari Baada ya Kifo cha Rodha George .Huu ni msiba wa pili mkubwa kwa wilaya ya Nyasa Mkoa wa Ruvuma Baada ya Jana aliyekuwa katibu wa wilaya ya Nyasa ambae inadaiwa alikuwa shabiki na msaada mkubwa kwa mbunge Komba Rhoda George kufariki dunia katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment