Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Wednesday, 4 February 2015

SAMATA AIKOSA CSKA

Mshambuliaji wa TP Mazembe na Taifa Stars, Mbwana Samatta ameshindwa jaribio la kucheza soka Ulaya kwenye klabu ya CSKA Moscow ya Russia baada ya ofa yao kushindikikana kabla ya dirisha la usajili kufungwa.Mwezi uliopita, Samatta alikwenda kufanya majaribio ya kucheza soka kwenye klabu hiyo ya  Russia  kwa siku saba na kufanikiwa, lakini mazungumzo baina  ya CSKA na TP Mazembe yalikwenda taratibu na kukwamisha suala hilo. Akizungumzia  suala hilo, Samatta alisema tatizo kubwa lililokwamisha dili hilo ni mawazo finyu ya klabu za Ulaya kwamba wachezaji wa Afrika ni wa bei rahisi, hivyo hata ofa waliyoitoa kwa klabu yake itakuwa ndogo. “Usajili ulifungwa mwisho wa Januari, dili lilitakiwa kukamilika kabla ya hapo lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo, tatizo wale walidhani nitakuwa mchezaji wa bei rahisi. “Tatizo jingine ni kwamba upepo unaonyesha bosi Moise Katumbi hataweza kuniruhusu kwa sasa, hata ikiwa hivyo lazima apokee fedha za maana,” alisema Samatta. “Sijakata tamaa bado, nasubiri usajili wa dirisha kubwa nirudi tena kujaribu bahati, kuna klabu nyingine za Ubelgiji na nchi nyingine za Ulaya

No comments:

Post a Comment