Wezesha
kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com
Friday, 20 March 2015
BARABARA YA MSIMBAZI KUFUNGWA
TANGAZO KWA UMMA KUTOKA DART NA TANROADS.
STRABAG WANAENDELEA KUJENGA BARABARA ZETU.
Kuanzia tarehe 01/04/2015 saa 07:00 AM barabara ya Msimbazi kuanzia Fire hadi Kamata itafungwa rasmi ili kupisha ujenzi wa barabara za mfumo wa DART. Barabara hiyo itajenngwa kwa Awamu tatu kutokana na Umuhimu wake. Awamu ya kwanza kipande cha kuanzia Makutano ya Barabara ya Morogoro hadi Mtaa wa Mkunguni (Msimbazi Polisi). Awamu ya Pili ni kuanzia Mkunguni hadi Barabara ya Uhuru (Keep left) na kumalizia Kipande cha Round about hadi Makutano ya Msimbazi na Nyerere eneo la Kamata.
Kwa Taarifa hii tafadhali zingatia maelekezo yatakayokuwa yakitolewa mara kwa mara kupitia vyombo mbalimbali vya habari na gari la matangazo ili kukupunguzia usumbufu wa Kuingia Kariakoo.
TUNAJENGA KWA AJILI YAKO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment