Habari zilizotufikia hivi punde zinaarifu kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba amefariki dunia.
Akidhibitisha kutokea kwa kifo hicho Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim amesema Mufti amefikwa na umauti hii leo asubuhi.
"Ni kweli Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba amefariki hii leo asubuhi kwa maradhi ya sukari na presha," alisema kwa ufupi Sheikh Alhhadi.
Kuhusu taratibu za mazishi amesema taarifa kamili zitatolewa muda si mrefu.
INNA LILLAH WA INNA ILLAHI RAJIUN.
No comments:
Post a Comment