Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Thursday, 22 January 2015

MISAMAHA YA KODI YAZIDI



Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)  inadaiwa kusababisha misamaha ya kodi kuzidi kupaa nchini Tanzania. Hatua hiyo  inafuatia  Rais kuto  saini sheria  hiyo  jambo linalopelekea  kukithiri kwa misamaha hiyo nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa  mwenyekiti wa  kamati hiyo, Kabwe Zitto  wakati akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dares salaam jana kuhusu  kauli ya Ikulu kushangazwa na kamati hiyo kuendelea kulalamikia misamaha ya kodi, wakati wameshindwa kupitisha muswada wa Sheria utakaosaidia kufuta misamaha ya kodi nchini.
Mwenyekiti huyo amesema “Si kweli kwamba hatujapitisha sheria, Mkurugenzi wa Ikulu aangalie taarifa zake vizuri, Sheria hii tayari imepitishwa ila mpaka sasa haijatekelezwa na ndio maana madhara ya misamaha ya kodi inazidi kuendelea,”
Ameongeza kuwa  taarifa ya  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inaonesha  kuzidi kupanda kwa misamaha ya kodi ambayo imefikia kiasi cha Sh trilioni 1.82 kwa mwaka wa fedha 2013/ 2014.
Zitto amemwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) awasiliane na Serikali ili kubaini chanzo na sababu zinazofanya sheria kutotangazwa kwenye gazeti la Serikali.
Kamati hiyo imemuagiza Waziri wa Fedha kuitangaza Sheria hiyo kwenye gazeti la Serikali ili iweze kutekelezwa. Sheria hiyo ya VAT iliyotakiwa kutekelezwa tangu Januari mwaka huu, ina wigo mkubwa wa kupunguza tatizo  la misamaha ya kodi endapo Serikal itaifanyia kazi mapema.

No comments:

Post a Comment