Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Saturday, 24 January 2015

MUHONGO AJIUZULU


Aliyekua Waziri wa Nishati na madini Sospeter Muhongo Amejiuzulu Wadhifa wake wa Uwaziri Katika mkutano wake wa waandishi wa habari aliouitisha.  Profesa huyo msomi wa masuala ya miamba nchini ameamua auachia ngazi nafasi yake akidai anawaachia wengine kwenye nafasi hiyo kutokana na watu waameacha kuzungumzia masuala ya maendeleo wanazungumzia mambo ya Escrow huku yeye hahusiki.Profesa Muhongo aliongeza kuwa hata mkataba wa Escrow ambao Ndio umeleta yote hayo anasema yeye hakuwepo wakati mkataba huo unasahiniwa
Mimi nashangaa leo watu kila kona wanaaona mimi nai mwizi, yaani kama mimi Ndio nimechukua mabilioni ya escrow wakati ukweli hupo wazi wakati wizara ya nisharti inaingia kwenye mkataba huo mimi sikuwepo kwenye nafasi ya uwaziri, lakini leo watu wananiona mimi ni mwiziAcha niaachia ngazi nafasi hii ya uwaziri kwani imekuwa ni shida sana, Mimi ni umbrella msomi nimepata tuzo sehemu mbalimbali duniani nasifika kwa kutoa ushahuri wenye tija, lakini leo naonekana mwizi, wakati kiihistoria yangu mimi ni umbrella msafi Sina Doa, Rangi wala sijawai hata kumwibia mtu , lakini watu wananiona mimi mwizi "alisema Profesa Muhongo.Aidha, Profesa Muhongo alisema Kabla hajafikia hatua ya kutangaza kujiuzulu aliwasiliana na  Rais Jakaya Kikwete alimuleze hatua nayotaka kuchukua ya kujiuzulu  Rais akakubali kujiuzulu Kwake.Vilevile Profesa Muhongo aliendelea kukanusha kile kilichotajwa  Ripoti ya PAC iliyomtuhumu kwamba yeye alikuwa Dalali Kati ya anayejiita mmiliki wa IPTL ambayo Sasa nai  Bwana Seith  Mkurugenzi wa VIP Engineering Bwana James Rugimalira kusema Kamati hiyo imemuonea.Kujiuzulu huku kwa Profesa Muhongo kunatokana mashinikizo mbalimbali kutoka ndani ya nchi hususani Bunge pamoja na   nchi wahisani ambao waligoma kutoa fedha za bajeti wakitaka waliohusika na ufisadi wa Bilioni 320 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa benki kuu BOT wachukuliwe hatua.

No comments:

Post a Comment