Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Friday, 23 January 2015

SAMATA AULA ULAYA


Habari nimezipata hivi punde zinasema kuwa Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samata amefanikiwa katika majaribio ya awali ya kujiunga na klabu ya Ligi kuu ya Russia CSKA Moscow.Samata yuko katika kambi ya timu hiyo iliyoko Spain akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha CSKA klabu ambayo inakamata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nchini Russia na ilishiriki Ligi ya mabingwa msimu huu ikiwa kundi moja na Bayern Munich,Manchester City na AS Roma.Hii inaweza kuwa habari njema kwa Samata na Tanzania kwa ujumla na kinachosubiriwa kusikiwa na Wapenda Soka hivi sasa ni kusikia taarifa rasmi toka kwa Klabu hiyo ya Moscow,TP Mazembe au Shirikisho la Soka nchini Tanzania TFF.

No comments:

Post a Comment