Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Monday, 12 January 2015

SHEIN NA MAPINDUZI LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kuongoza maadhimisho ya miaka hamsini na moja ya mapinduzi. Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hii leo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka hamsini na moja ya mapinduzi tukufu yaliyomaliza utawala wa Kisultani visiwani humo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ataongoza sherehe hizo ambazo pia zitahudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya nchi. Katika hatua nyingine wananchi wametakiwa kushiriki kikamilifu na kuonesha umoja na mshikamano walionao katika sherehe hizo za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Karume.

No comments:

Post a Comment