VIONGOZI wa dini ya Kiislamu wamepinga tamko lililotolewa na Jukwaa la Wakristo
kuhusu sheria hiyo ya kuanzishwa Mahakama ya Kadhi na kudai kuwa matamko ya
aina hiyo yanaweza kusababisha machafuko nchini.Kauli hiyo zimekuja siku moja
baada ya Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) kutoa waraka, likipinga muswada
unaopendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi unaotarajiwa kuwasilishwa bungeni
wakati wowote.Akizungumza na
Chanzo chetu Imamu wa Msikiti wa Idrisa
uliopo Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Sheikh Ally Basalehe alisema viongozi wa
dini ya Kikristo mara nyingi wamekuwa wakipinga masuala mbalimbali yanayogusa
Uislamu yakiwamo yale mazuri.Alisema mwenendo wa kupinga
masuala ya kidini sio mzuri, kwani Waislamu hawajatamka kuwa sheria za dini
hiyo zitawale nchini isipokuwa mahakama hiyo itajali masuala muhimu yakiwamo ya
ndoa na mirathi Kwa upande wake Msemaji wa Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Rajabu Katimba, alikiambia Chanzo chetu
kwa njia ya simu jana kuwa kwa Waislamu Mahakama ya Kadhi ni ibada kama ibada
nyingine, na haipaswi kupingwa na chombo kingine cha dini kutokana na umuhimu
wake.“Tunawashangaa viongozi wa dini
ya Kikristo kusema suala hili ni la kibaguzi, mbona Serikali imeingia mkataba
na hospitali za makanisa mwaka 1992 na wanapewa mabilioni ya fedha za kodi za
Watanzania wakiwamo Waislamu sisi hatujawahi kuhoji wala kulalamika?” alihoji
Sheikh Katimba.
No comments:
Post a Comment