Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Monday, 9 February 2015

IVORY COAST BINGWA AFRIKA 2015


Hapo Jana Shujaa wa Ivory Coast ni Kipa wao Boubacar Barry ambae aliokoa na pia kufunga Penati muhimu iliyowapa Ivory Coast Ubingwa.Kila Timu ilikosa Penati 5 na ndipo Kipa Barry akaokoa Penati iliyopigwa na Kipa mwenzake Brimah Razak na kisha kufunga Penati ya ushindi.Kwa Kocha wa Ghana, Avram Grant, hii ni mara ya pili kushindwa Fainali kubwa kwa Mikwaju ya Penati baada ya Mwaka 2008, akiwa na Chelsea, alipobwagwa kwa Mikwaju ya Penati na Manchester United kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Moscow, Urusi.Ghana, ambao mara ya mwisho kati ya mara zao 4 kuwa Bingwa wa Afrika ilikuwa 1982, wangeweza kushinda Fainali hii hasa baada ya kupata nafasi kadhaa katika Dakika 120 za Mchezo na mara mbili kupiga Posti.Pia hata kwenye Mikwaju ya Penati walianza kwa mguu mzuri pale Ivory Coast walipokosa Penati zao 2 za kwanza kwa Mchezaji mpya wa Manchester City, Wilfried Bony, kupiga Posti na Junior Tallo kutoa nje lakini Ghana nao, kupitia Afriyie Acquah na Frank Acheampong, wakakosa.Baada ya Wachezaji wote wa ndani kumaliza kupiga Penati zao ikaja zamu za Makipa na ndipo Kipa Boubacar Barry akaokoa Penati iliyopigwa na Kipa mwenzake Brimah Razak na kisha kufunga Penati ya ushindi kwa Ivory Coast kutwaa Ubingwa kwa Penati 9-8.VIKOSI:Ivory Coast: Barry, Kolo Toure, Tiene (Kalou - 116'), Gervinho (Gadji-Celi Carmel Junior - 122'), Bony, Gradel (Doumbia - 67'), Aurier, Yaya Toure, Gonzaroua Die, Bailly, Kanon.Ghana: Brimah, Afful, Rahman, Mensah, Boye, Wakaso, Acquah, Ayew, Atsu (Acheampong - 116'), Gyan (Badu - 121'), Appiah J.Ayew - 99').REFA: Bakary Papa Gassama
Chini baadhi ya matukio ya mchezo huo






No comments:

Post a Comment