Hali tete na taharuki imezuka katika Jiji la Tanga kuanzia jana baada ya kusikika milio na mabomu na risasi zilizokuwa zikirushwa wakati vikosi vya jeshi la polisi na JWTZ vikishambuliana na kundi linalodaiwa kuwa ni la majambazi.
Milio hiyo imesababisha baadhi ya wakazi wa
kitongoji cha Karasha Amboni Jijini Tanga kulazimika kuhama makazi
kusalimisha uhai wao huku askari sita wa jeshi la wananchi (JWTZ) na wa
polisi wakidaiwa kujeruhiwa vibaya.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga leo
Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja amesema kuwa
hiyo ilikuwa ni oparesheni ya ushirikiano wa Polisi na jeshi, JWTZ lengo
likiwa ni kudhibiti uhalifu nchini.
“Baada ya askari kufika mapangoni, kundi la
majambazi lilianza kufanya mashambulizi ya risasi na katika majibizano,
askari sita walijeruhiwa na kuwahishwa katika hospitali ya Mkoa wa
Tanga ya Bombo,” amesema Kamishna Chagonja.
Shuhuda mmoja ambaye ni mkazi wa eneo hilo, Rehema
Juma (34) amesema yeye na mwenzake walilazimika kuhama kwenye nyumba
zao kukimbia mapigano hayo kwa kuhofia maisha yao
“Kilichosababisha tuhame ni milio ya mabomu na
risasi na baadaye tukaona helikopta ikirandaranda tukapata hofu kubwa...
hatuwezi tena kutoka kwenye nyumba zetu,” amesema Rehema Juma ambaye
yeye na watoto wake watatu wamelazimika kuhifadhiwa kwa ndugu zake mtaa
wa Amboni.
No comments:
Post a Comment