Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Monday, 23 March 2015

KIKWETE UHURU WAMALIZA TOFAUTI

Rais Jakaya Kikwete, na Rais wa kenya Uhuru Kenyata. Marais hao walifanya mazungumzo ya kidiplomasian kuhusu mvutano wa safari za magari ya kitalii ya Tanzania kupigwa stop kuingia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, ambapo Tanzania nayo nkama msemo wa kiswahili usemavyo, "Ukimwaga mboga tunamwaga ugali" na kujibu mapigo kwa kupunguza safari za shirika la ndege la Kenya KQ, kuingia anga la Tanzania kutoka safari za awali 42 kwa wiki hadi 14. Hali hiyo imeishtua serikali ya Kenya na hivyo kuamua kiutu uzima kufanya mazungumzo baina ya wakubwa hao wawili baada ya maafisa kutoka Kenya kususia kikao cha usuluhishi baina ya pande hizo mbili jijini Arusha juzi. Sasa safari hizo zimeruhusiwa kuanzia leo saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe, aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo alasiri, Jumapili Machi 22, 2015

No comments:

Post a Comment