Aliyekuwa Waziri wa viwanda na biashara Dr Abdallah Kigoda amefariki dunia nchini India.
Kwa mujibu wa taarifa iliyothibishwa na katibu wa bunge Thomas Kashilila, Dr Kigoda amefariki dunia nchini India alikokuwa amelazwa kwa wiki kadhaa.Taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuurejesha nchini tayari kwa mazishi zinaendelea.
Dr Kigoda alikuwa ni mgombea wa ubunge jimbo la Handeni kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi na ni mgombea wa nne kufariki ndani ya mwezi mmoja.
No comments:
Post a Comment