Wezesha
kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com
Wednesday, 14 January 2015
SAMATA KUKIPIGA ULAYA
Huenda utakuwa ni mwaka wa neema kwa mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP
Mazembe kwa kuwa timu nne za Ulaya zimeonyesha nia ya kumchukua,
ambazo ni kutoka katika nchi za Ufaransa na Italia, zimeonyesha nia ya
kufanya kazi na mshambuliaji huyo Mtanzania.
“Kweli tunayajua majina ya timu nne, kumekuwa na mawasiliano kupitia
meneja wake Tanzania pamoja na uongozi wa TP Mazembe,” kilieleza chanzo
kutoka Ufaransa.
“Tusingependa kuanza kueleza kila kilichopo kwa sasa, lakini tunaamini
Samatta anaondoka Mazembe msimu huu.”
Baada ya taarifa hizo, juhudi zilifanyika kumpata meneja wake, Jamal
Kisongo ambaye alitoa ushirikiano.
“Kweli kuna timu zinamhitaji, kama nilivyokueleza awali Mbwana si mtu wa
kwenda kufanya majaribio, badala yake kujiunga na timu na kuanza kazi.
“Sasa kinachofanyika ni taratibu na nimekuwa na mawasiliano na uongozi
wa TP Mazembe, hivyo vuteni subira kidogo,” alisema Kisongo akionyesha
kujiamini kuhusiana na mchezaji wake huyo.
Samatta yupo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mapumziko na amekuwa
mchezaji tegemeo wa kikosi cha Mazembe.
Awali ilielezwa, mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi, alikuwa akifanya
juhudi kuhakikisha Samatta anabaki Lubumbashi, DR Congo, lakini Kisongo
amehakikisha anakwenda mbele zaidi ili kupata mafanikio zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment