Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Friday, 6 March 2015

ALBINO WAZUA BALAA IKULU

Watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), leo walizusha vurugu katika viwanja vya Ikulu wakipinga baadhi ya wao kuonana na Rais Jakaya Kikwete.Kundi la albino waliokuwa wamebaki nje walianza kupaza sauti na kudai waliopewa nafasi ya kuingia kuonana na Mhe. Rais si viongozi wao, jambo ambalo liliwalazimu maofisa usalama kuingilia kati.Katika mkutano huo, Rais Kikwete alikutana na wawakilishi 15 huku wengine zaidi ya 30 wakiwa nje na kuanza kupaza sauti zao na kusema kuwa walioingia ndani sio viongozi wao kwani muda wao ulishakwisha hivyo ni bora wakatoka kabla hawajaanzisha vurugu kubwa katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment