Wezesha

kama una maoni au habari tafadhali tutumie kwa kupitia email yetu.shanellally@gmail.com

Wednesday, 4 March 2015

KOMBA AZIKWA RUVUMA

Safari ya Komba, iliyoanza miaka 61 iliyopita kwenye kijiji cha Lituhi ambako aliazikwa jana, ilikamilishwa kwa salamu mbalimbali ambazo zilielezea ushupavu wa kapteni huyo mstaafu wa jeshi.Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wananchi, wakiwamo viongozi mbalimbaliwakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete na mkewe Salma, yalifanyika katika makaburi ya Misheni,katika Kijiji cha Lituhi (Bundi) wilayani Nyasa mkoani Ruvuma.Nyuso za majonzi zilitawala kwa waombolezaji waliojitokeza nyumbani kwa marehemu, takriban mita 500 kutoka katika makaburi hayo na baadaye katika misa iliyofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Lituhi, ikiongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki la Mbinga.Kaimu katibu wa Bunge, John Joel, akisoma wasifu wa marehemu, alisema Kapteni Komba aliyefariki dunia Februari 28, mwaka huu akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam, alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na mara kadhaa Ofisi ya Bunge ilimpeleka India kwa matibabu. Pia alikuwa na tatizo la kisukari ambalo ndilo lililochukua maisha yake.Mazishi hayo yalishuhudiwa na viongozi mbalimbali, akiwamo Edward Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Utaratibu na Bunge), Jenister Mhagama na mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi.Wengine ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Ali Abdallah Ali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Spika wa Bunge, Anne Makinda. Picha za mazishi chini

No comments:

Post a Comment