BARAZA Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) limemteua Sheikh Abubakar Zuber bin Ally, kukaimu nafasi ya aliyekuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban Simba, aliyefariki dunia Juni 15 mwaka huu.
Akizungumza na wanahabari, mjumbe wa Baraza la Ulamaa Bakwata na Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheik Hamid Masoud Jongo, amesema Sheikh Abuubakar atakaimu nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu baada ya hapo utafanyika uchaguzi wa kiongozi ambaye atashika madaraka, lakini akaongeza kuwa wameamua kumteua mufti huyo kutokana na sifa alizo kuwa nazo za uongozi ikiwemo elimu, mwamko na kujitambua.
No comments:
Post a Comment